TANZANIA VOLUNTEERS FOR DEVELOPMENT
Location
City/Region: Dar es Salaam
District: Temeke
Street: Tuangoma Masaki
About The Company
TAVODE ni Shirika lisilo la kiserikali (NGO) lililosajiliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1999 kwa jina la Tanzania Volunteer Services Movement (TVSM) na baadaye mwaka 2006 kubadilisha jina na kuitwa Tanzania Volunteers For Development Trust (TAVODET) na kupewa hati ya usajili No. 1907 ya 24/07/2006 chini ya Sheria ya The Trustees Incorporation Act (Cap 318 R.E. 2002). Hata hivyo mwaka 2019 kutokana na muongozo wa Wizara husika Shirika lililazimika kuomba cheti cha ukubalifu na kupewa usajili mpya No. 00NGO/R2/000051 ya 15/07/2019 chini ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya kiserikali No. 24 ya mwaka 2002 kifungu cha 12(2) kwa jina jipya la Tanzania Volunteers For Development (TAVODE).
Lengo kuu la Shirika hili toka mwanzo ilikuwa ni kuhamasisha na kutoa elimu ya moyo wa kufanya kazi za kujitolea (Volunteerism) na kutoa huduma mbalimbali za kijamii kwa jumuia ya watanzania ikiwemo kuanzisha miradi mbalimbali ya huduma za kijamii kwa gharama za chini kwa njia ya kujitolea.